Manchester City Kudaiwa Zaidi Ya £200m Wakikutwa Na Hatia

Manchester City inaweza kukumbana na madai makubwa ya fidia kutoka kwa klabu pinzani baada ya kupatikana na hatia katika tuhuma za kuvunja kanuni za kifedha za Premier League, huku thamani ya madai hayo ikikadiriwa kuzidi £200 milioni kwa baadhi ya klabu.

Kwa mujibu wa vyanzo vinavyofahamu mchakato huo, klabu kadhaa zimeanza kuandaa njia za kisheria zikisubiri uamuzi wa kesi hiyo iliyodumu kwa miaka kadhaa. Arsenal, Manchester United, Liverpool na Tottenham Hotspur ni miongoni mwa klabu ambazo zimeripotiwa kuhifadhi haki zao za kudai fidia chini ya Kifungu W cha kanuni za mashindano.

Hatua hiyo iliwezesha klabu hizo kulinda haki yao ya kufungua madai ya fidia kabla ya muda wa kisheria wa kuwasilisha kesi hizo kumalizika. Arsenal inaripotiwa kuwa klabu ya kwanza kuhifadhi haki hiyo, kabla ya Tottenham, Liverpool na Manchester United kufuata.

Kesi hiyo inaweza kufungua mlango wa madai yanayohusisha hasara za mapato ambazo klabu hizo zinadai zingeweza kupata kama Manchester City isingekuwa imepata mafanikio yaliyotajwa kwenye tuhuma hizo. Kwa mfano, Manchester United ilikosa kutwaa mataji ya Premier League ya 2011/12 na 2017/18, huku Liverpool ikikosa taji la 2013/14, wakati City ilipokuwa ikifuzu Ligi ya Mabingwa mara kwa mara katika kipindi kinachochunguzwa.

Hata hivyo, madai hayo huenda yasiishie kwenye misimu ambayo klabu hizo zilipoteza nafasi ya kutwaa mataji au mapato ya moja kwa moja. Wanasheria wanaweza pia kujaribu kudai kile kinachoitwa loss of chance, yaani hasara iliyotokana na kupoteza fursa za mafanikio katika misimu iliyofuata, pamoja na uwezekano wa kupoteza mikataba ya kibiashara.

Manchester City Kudaiwa Zaidi Ya £200m Wakikutwa Na Hatia

Mfano muhimu wa kesi kama hiyo ulitokea Juni mwaka huu, wakati Burnley ilipofanikiwa kudai fidia kutoka Everton. Tume huru iliamuru Everton kulipa £35.1 milioni baada ya kukutwa kuwa ilikiuka kanuni za Profit and Sustainability Rules msimu wa 2021/22, hali iliyodaiwa kuipa klabu hiyo faida ya kimichezo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Everton ilimaliza nafasi ya 16 ikiwa na pointi 39 na kubaki Premier League, huku Burnley ikishuka daraja baada ya kumaliza nafasi ya 18 ikiwa na pointi 35. Kesi hiyo sasa inaweza kuwa rejea muhimu kwa klabu zitakazojaribu kufungua madai dhidi ya City.

Hata hivyo, hatua yoyote ya kisheria dhidi ya Manchester City haiwezi kuanza kabla ya kesi nzima kumalizika pamoja na mchakato wa rufaa. Manchester City inatarajiwa kutumia kila njia ya kisheria kupinga uamuzi wowote wa kuikuta na hatia, hasa kutokana na ukubwa wa madai yanayohusishwa na kesi hiyo.

Manchester City Kudaiwa Zaidi Ya £200m Wakikutwa Na Hatia

Manchester City tayari imesisitiza msimamo wake kwamba bado haijapatikana na hatia, ikikumbusha kuwa mchakato wa Premier League bado unaendelea na kwamba vipengele muhimu vya kesi hiyo havijakamilika.

Klabu hiyo pia imesema imeheshimu mchakato huo kwa miaka minane kwa matarajio kwamba bodi na uongozi wa Premier League wataendesha kesi hiyo kama wasimamizi huru, wasio na upendeleo na wenye haki.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.