Manchester City Mbioni Kukamilisha dili la Gvardiol

Klabu ya Manchester City wako mbioni kukamilisha dili la beki wa kimataifa wa Croatia anayekipiga katika klabu ya Rb Leipzig ya nchini Ujerumani Josko Gvardiol.

Manchester City walishamalizana na beki huyo siku kumi nyuma lakini dili hilo bado halijakamilika kutokana na upande wa klabu ya Rb Leipzig, Ikiwa ndio kitu ambacho mabingwa hao wa ulaya wanakifanyia kwasasa.manchester cityKlabu ya Leipzig na Man City wanatarajiwa kukamilisha usajili wa beki huyo mwishoni mwa wiki hii, Ambapo kutakua na mgawanyo pia wa kimaslahi kwa klabu ya Dinamo Zagreb ambayo ndio iliyomkuza beki huyo.

Josko Gvardiol amekua akifuatiliwa na vilabu kadhaa barani ulaya lakini Man City ndio wamefanikiwa kufikia makubaliano na beki huyo mwenye ubora wa hali ya juu anayesifika kwa uwezo wake kupiga pasi kwa usahihi.manchester cityKlabu ya Manchester City wanaboresha eneo lao la ulinzi ambalo kuna hatihati ya kuwakosa mabeki kadhaa kama Joao Cancelo, Kylie Walker, na Aymeric Laporte ambao wanahitajika

Acha ujumbe