Manchester City Waendeleza Wimbi la Ushindi

Klabu ya Manchester City wameendeleza wimbi la ushindi katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kufanikiwa kuifunga klabu ya Sheffield United kwa mabao mawili kwa moja.

Mabao ya Earling Haaland na kiungo Rodri ndio yameiwezesha klabu hiyo kupata alama tatu muhimu katika mchezo wa leo ambao ulionekana kua mgumu kwa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Uingereza kutokana na namna wapinzani wao walivyocheza.manchester CitySheffield United walifanikiwa kucheza kwa nidhamu sana na kuhakikisha wazuia vizuri dhidi ya Man City na mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika walikua hawajarusu bao licha ya mshambuliaji Earling Haaland kukosa mkwaju wa penati.

Kipindi cha pili Man City waliendelea kuliandama lango la Sheffield kwa kiwango kikubwa mpaka pale dakika ya 63 ya mchezo Earling Haaland kuwapa City bao la utangulizi kabla ya Sheffield kusawazisha bao hilo dakika ya Jayden Bogle kusawazisha na matokeo kua moja kwa moja.manchester CityKlabu ya Manchester City walijihakikishia alama tatu muhimu baada ya kiungo wake Rodri kupiga mkwaju mkali mnamo dakika ya 88 ya mchezo na kufunga bao lilihakikisha mabingwa hao watetezi wanaondoka na alama zote tatu.

Acha ujumbe