Manchester City wao wanaendelea kutembeza vichapo tu katika ligi kuu ya Uingereza ambapo leo wamefanikiwa kushinda kwa jumla ya mabao matatu kwa moja dhidi ya klabu Westham United.
Manchester City wao wameendeleza ushindi kwa aslimia 100 mpaka sasa baada ya kuifunga klabu ya Westham United wakiwa katika dimba lao la nyumbani na kufanikiwa kushinda michezo yao yote mpaka sasa.Vijana wa Pep Guardiola walitanguliwa kwa bao moja kwa bila katika mchezo huo mpaka unakwenda mapumziko goli la Westham likifungwa na kiungo mpya wa timu hiyo James Ward Prowse.
Kipindi cha pili Man City walikuja na sura ya tofauti kwani walianza kwa kushambulia kwa kasi wakihitaji bao la kusawazisha na walifanikiwa kulipata kupitia winga mpya wa klabu hiyo Jeremy Doku mapema tu dakika ya 46 na kuufanya ubao kusoma bao moja kwa moja.Klabu ya Manchester City waliendelea kufanya msako katika mchezo huo ambapo walifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa kiungo Bernardo Silva, Huku bao la tatu likifungwa na mshambuliaji wao matata Earling Haaland na Man City wakiendelea kukaa kileleni wakiwa na alama 15 baada ya kushinda michezo yao yote mitano.