Manchester City Yaibukia kwa Rice

Klabu ya Manchester City imeingia kwenye vita ya kumsajili kiungo wa klabu ya West Ham United Declan Rice ambaye amekua akifukuziwa kwa karibu na klabu Arsenal.

Manchester City imeondokewa na kiungo wake Ilkay Gundogan ambaye ameenda klabu ya Barcelona, Hivo mabingwa hao wa soka kutoka nchini Uingereza wanatafuta mbadala wa kiungo huyo na Rice ndio limekua chaguo la kwanza.Manchester CityDeclan Rice amekua mchezaji anayepiganiwa zaidi katika dirisha hili kwani klabu ya Arsenal wameonesha uhitaji mkubwa kwa kiungo huyo huku wakipelekea ofa mbili ambazo zote zimepigwa chini, Lakini City wameripotiwa kupeleka ofa yao ya kwanza leo.

Manchester City wamekua na ushawishi mkubwa katika soka la usajili miaka ya hivi karibuni ambapo wamekua wakitoa pesa ya kutosha ya usajili, Lakini pia wachezaji wamekua wakitaka kujiunga na timu hiyo kwani wanakua na uhakika wa kushinda mataji.Manchester CityArsenal bado wanaamini wanaweza kumbeba kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza, Lakini Manchestert City kujiunga kwenye mbio hizo imekua tishio kubwa kwa washika mitutu hao wa London kwani City wamekua na ushawishi mkubwa sokoni.

Acha ujumbe