Klabu ya Manchester City imefanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Uingereza baada ya kupata ushindi dhidi ya klabu ya Fulham katika dimba la Etihad mapema leo.

Klabu hiyo ambayo imepata ushindi wake wa 10 kwenye michezo 13 ya ligi kuu ya Uingereza baada ya kuifunga klabu ya Fulham Man City wamekaa kileleni mwa ligi hiyo wakuiwashusha klabu ya Arsenal.

Mchezo uliokua mgumu sana kwa klabu ya Manchester City baada ya Julian Alvarez kufunga bao la kuongoza dakika chache beki Joao Cancelo alifanya madhambi ndani ya boksi na kusababisha mkwaju wa penati ambao ulifungwa na Andreas Perreyra huku yeye akipewa kadi nyekundu.manchester cityBaada ya beki huyo kuoneshwa kadi nyekundu ikafanya mchezo huo kua mgumu kwa klabu ya Man City mpaka pale ambapo walihitajika kusubiri dakika za nyongeza na kiungo wa klabu hiyo Kevin De Bruyne kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari na klabu hiyo kupata mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na mshambuliaji Earling Halaand akietoka kwenye majeraha.

Klabu ya Manchester City imefanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa alama moja baada ya kufikisha alama 32 huku Arsenal wakiwa na alama 31. Pia klabu ya Arsenal wao wakiwa nyuma kwa mchezo mmoja ambapo kesho watacheza na klabu ya Chelsea.

aviatorUlishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa