Klabu ya Manchester City imefanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kufanikiwa kuifunga klabu ya Luton Town kwa jumla ya mabao matano kwa moja.
Manchester City ambao wako kwenye mbio za ubingwa za ligi kuu ya Uingereza wakikimbizana na klabu za Liverpool pamoja na Arsenal ambao wanakamata nafasi ya pili mpaka sasa.Mchezo wa leo ulikua muhimu kwa klabu ya Man City kwajili ya kuendelea kubaki kwenye mbio za ubingwa wa Uingereza kwa mara ya nne mfululizo, Ikiwa sababu ya kuonekana kushambulia kuanzia mwanzo na kutafuta magoli mapema ambapo dakika ya 2 tu beki Hashioka anajifunga baada ya kubabatizwa na shuti lililopigwa na Earling Haaland.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa City kuongoza kwa bao moja kwa bila ila kipindi cha pili mambo yote ndio yalibadilika kwani vijana wa Pep Guardiola walifanikiwa kupata mabao manne ambapo alikua Mateo Kovacic dakika ya 64 aliongeza goli la pili, dakika ya 76 Haaland akifunga bao la tatu kwa mkwaju wa penati dakika ya 87 na 93 mabao mawili yalifungwa na Jeremy Doku na Josko Gvardiol na kufanya mabao kufika matano.Bao pekee la kufutia machozi kwa upande Luton lilifungwa na Ross Barkley dakika ya 81 ya mchezo, Manchester City wanafanikiwa kufikisha alama 73huku wakiwa mbele kwa mchezo mmoja kwa wapinzani wake Liverpool na Arsenal ambao wanacheza kesho matokeo yao yakiwa mazuri basi City atashuka kileleni lakini wakipata matokeo mabaya basi Man City watabaki kileleni.