Klabu ya Manchester City imetawala tena kwenye orodha ya wachezaji wa kiume wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Fifa ambazo zinatarajiwa kutolewa hivi karibuni.
Manchester City imefanikiwa kutoa wachezaji sita ambao wapo kwenye orodha hiyo ya shirikisho la soka duniani wakiongozwa na Earling Haaland, Kevin de Bruyne,Bernardo Silva, Rodri, Julian Alvarez, na kiungo mpya klabuni hapo Declan Rice.Klabu hiyo imefanikiwa kutoa idadi kubwa ya wachezaji kwenye orodha ya tuzo hizo kutokana na ubora ambao klabu hiyo iliuonesha msimu uliomalizika na kufanikiwa kutwaa mataji matatu ndani ya msimu mmoja.
Mshambuliaji matata ndani ya klabu hiyo Earling Haaland anapewa nafasi ya kutwaa tuzo hiyo kutokana ubora mkubwa ambao amekua nao msimu uliomalizika mpaka sasa na alikua miongoni mwa wachezaji waliotoa mchango mkubwa kwa Man City kutwaa mataji matatu msimu uliomalizika.Klabu ya Manchester City ilifanikiwa kutawala katika orodha ya tuzo za Ballon Dor kama ambavyo wamefanya awamu hii katika tuzo za Fifa, Huku sababu ikiwa ni ileile ambayo ni ubora mkubwa ambayo klabu hiyo imekua nayo msimu uliomalizika.