Klabu ya Manchester City wamekubali kutoa kiasi cha £42million ili kufanikisha usajiri wa kiungo wa klabu ya Leeds United Kalvin Phillips huku wakikubali kuongeza kiasi cha £3 million kwenye ada ya uhamisho huo.

Kuna taarifa kuwa Kalvin Phillips na Manchester City tayari wameshakubalina makubaliano binafsi, sasa imebaki kwa upande wa klabu ya Leeds United kufanya hitimisho kwa kumuachia ili aweze kujiunga na mabingwa hao.

Manchester City

Pep Guardiola anataka kuimarisha safu yake ya kiungo, baada ya kiungo wake mahiri wa kimataifa kutoka Brazili Fernandinho kuachana na klabu ya Manchester City mwishoni mwa msimu.

Kalvin Phillips awali alikuwa anahitajika na klabu ya Manchester United na vilabu kadhaa vikubwa ndani ya Uingereza.

Pia klabu ya Manchester City imekubaliana na klabu ya Leeds, kuwauzia kiungo wake mwenye miaka 18 Darko Gyabi ambaye anatokea kwenye akademi ya City kuhamia Leeds kwa ada ya uhamishi wa £5 million, ambapo uhamisho wake ni tofauti kabisa na makubaliano Philips.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa