Manchester Derby nani kukufukia kwa mwenzake?

Leo unapigwa mchezo mkali pale kwenye ligi kuu ya Uingereza ambapo unakutanisha timu mbili kutoka jiji moja yaani Manchester derby ambapo Man city watakua nyumbani kuwakaribisha majirani zao Man United.

Hii kwasasa unaweza kusema ni derby ya wachovu kutokana na muendelezo ambao timu hizi mbili umekua nao siku za hivi karibuni kwani sio Man United wala Man City ambao wamekua kwenye ubora wao, Hivo mchezo wa leo unasubiriwa kwa hamu kujua ni timu gani ambayo inaweza kuonesha uhai au kufufukia mbele ya mwenzake.manchester derbyLicha ya kuonekana kama derby ya wachovu lakini bado ni mchezo ambao unatarajiwa kua na mvuto wa aina yake kutokana na ushindani ambao umekua baina ya timu hizi kama unavyojua huu ni mchezo wa mahasimu, Hivo haitajalisha timu ipi ni nzuri kuliko mwenzake mara zote hua unakua mchezo wenye ushindani mkubwa pale wanapokutana.

Miaka ya karibuni klabu ya Man United imeonekana kukumbana na vipigo vingi zaidi kwani katika michezo mitano ya mwisho wamefungwa michezo minne na kupata ushindi mchezo mmoja tu, Leo ni siku ambayo wanaweza kufuta uteja ambao wamekua nao miaka ya karibuni mbele ya mahasimu wao wa karibu kabisa.manchester derby

Man City nao bado wanaitafuta fomu yao kwani kwenye michezo kumi iliyopita wamepata ushindi mchezo mmoja tu huku wakisuluhu michezo miwili na kupoteza michezo saba, Hii ikiwa ni rekodi mbaya zaidi kwa upande wao baada ya miaka mingi kupita hivo Manchester derby leo itakua ni ya kila mmoja kutafuta namna ya kujaribu kurudi kwenye njia ya ushindi.

Acha ujumbe