Manchester Derby mchezo unaozikutanisha timu zinazotoka katika jiji la Manchester ambapo hua ni timu za Manchester United na Manchester city ambapo mchezo wao utapigwa leo katika dimba la Etihad.

manchester UnitedManchester Deby leo inakwenda kuwakutanisha makocha wawili ambao ni zao la gwiji wa zamani wa vilabu vya Ajax ya nchini Uholanzi na klabu ya Fc Barcelona ya nchini Hispania Johan Cruyff, Gwiji huyo ambae inaelezwa ndio muasisi wa mpira wa pasi fupifupi maarufu kama Tiktaka leo vijana wake wawili watamenyana katika dabi hiyo ambaye ni Pep Guardiola na Eric Ten Haag.

Makocha hao ambao wanafanana falsafa za kiuchezaji na wote wakimuangalia Cruyff kama mfano wao leo wanakwenda kukutana katika Manchester derby ikiwa ni mara yao ya kwanza kukutana kama wapinzani.

Ikumbukwe wakati kocha Pep Guardiola anafundisha klabu ya Fc Bayern Munich ya nchini Ujerumani Eric Ten Haag alikua kama kocha wa timu ya akiba ya klabu hiyo na inaelezwa Pep alikua anafurahishwa na uelewa wa Eric mpaka kuna wakati akawa anamuachia aongoze mazoezi ya timu hiyo.

manchester derbyLeo makocha hao wawili wanaosifika kwa mbinu na soka la kuvutia ambalo wamechukua kutoka kwa mwalimu wao Johan Cruyff watamenyana katika dimba la Etihad katika mida ya saa kumi kwa saa za Afrika mashariki.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa