Klabu ya Manchester United imemtambulisha mchezaji mpya ambaye wamekamilisha usajiri wake akiwa kama mchezaji huru aliyemaliza muda wake kwenye klabu ya Brentford fc Christian Eriksen.
Christian Eriksen amajiunga na Manchester United kwa kandarasi ya miaka mitatu, ambapo mkataba wake unatarajiwa kutamatika June 2025.
“Man United ni klabu maalum, na nina shauku ya kuanza kuitumikia. Ten Hag ni kocha bora. Nimefanya mazungumzo nae, Ninafurahia zaidi maisha ya baadae.” Alisema Eriksen
Eriksen baada ya kupata matatizo ya moyo kwenye mchezo wa Euro 2020, klabu yake ya Inter milan ilikuwa haina busi kuvunja mkataba wake kutokana na sheria za nchini italia kutoruhusu mchezaji aliyepandikizwa vifaa maalum kwa ajiri ya usaidizi.