Manchester United Bundi Aanza Kulia Mapema

Makala iliyopita
West Ham Wamalizana na Wan Bissaka
Wachezaji wawili ambao ni Rasmu Hojlund na Leny Yoro walipata majeraha katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya dhidi ya klabu ya Arsenal, Huku ikielezwa watakua nje kwa kipindi cha muda kidogo ambapo Leny Yoro atakua nje kwa miezi mitatu, Hojlund yeye atakaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita.
Klabu ya Manchester United kutokana na hiki ambacho kinaendelea kwasasa inaweza kuwapa nguvu ya kukamilisha sajili ambazo walikua wanataka kuzifanya mwanzoni lakini wakaonekana kama wamepunguza kasi, Kwasasa wanaelezwa wanataka kumaliza mapema dili la beki Mathijjs De LigtΒ kutokana na majeraha aliyoyapata Leny Yoro.