Manchester United Hawaongezi Hela kwa Mount

Klabu ya Manchester United imeripotiwa haina mpango wa kuongeza dau kwajili ya kiungo wa klabu ya Chelsea Mason Mount baada ya ofa yao ya tatu kukataliwa.

Chelsea wamekataa ofa tatu mpaka sasa za klabu ya Manchester United ambapo ofa ya mwisho ilikua paundi milioni 55, Huku Chelsea ikihitaji kiasi kisichopungua paundi milioni 60 kitu ambacho Man United wameonesha hawako tayari kukitoa.manchester UnitedKlabu ya Chelsea imeripotiwa kutoa fursa kwa klabu ya Man United na upande wa mchezaji na kuangalia namna wanaweza kutimiza mahitaji ya kila upande ili kuhakikisha dili hilo linakamilika na kila upande kunufaika.

Manchester United wakiwa hawana mpango wa kuongeza kiasi cha pesa kwa Chelsea lakini hawajitoa kwenye dili hili kama ilivyoripotiwa, Huku wakiamini bado wana nafasi ya kumchukua mchezaji huyo ndani ya viunga vya Stamford Bridge.manchester UnitedUpande wa mchezaji Mason Mount na uongozi wake wanaamini nafasi ya kuondoka na kujiunga na Manchester United ndani ya dirisha hili kubwa licha ya ofa ya klabu hiyo kupigwa chini, Kwani Mount ameshakubaliana na Man United maslahi binafsi siku kadhaa nyuma.

Acha ujumbe