Manchester United Kumsajili Rabiot

Klabu ya Manchester United inaelezwa ina mpango wa kumsajili kiungo wa zamani wa klabu ya Juventus raia wa kimataifa wa Ufaransa Andrien Rabiot kwa mipango ya muda mfupi kwa dili la ambalo wataweza kulilipa.

Kiungo Rabiot mpaka sasa yupo huru kwakua amemaliza mkataba wake na klabu ya Juventus na amepata ofa mbalimbali kutoka vilabu vya Uturuki na Saudia Arabia, Lakini inaelezwa mipango yake ni kucheza kwenye ligi kubwa tano barani ulaya ambazo ni Uingereza, Ujerumani, Italia, Hispania, pamoja na Ufaransa.manchester unitedManchester United wanamuona Rabiot kama mchezaji ambaye anaweza kuimarisha eneo lao la kiungo licha kumsajili mchezaji Manuel Ugarte kutoka klabu ya PSG, Hivo mpaka sasa inaelezwa kama mchezaji huyo atakubali ofa ambayo mashetani wekundu watampatia basi watamsajili.

Ikumbukwe klabu ya Manchester United iliwahi kumfukuzia kiungo huyo mwaka 2022 na dili lilivunjika baada ya kushindwana na mchezaji huyo kwenye maslahi binafsi, Kwasasa klabu hiyo inafanya mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji huyo kuangalia kama wataweza kuhimili malipo yake ili waweze kumsajili.

Acha ujumbe