Manchester United Kibaruani Goodson Park Leo

Klabu ya Manchester United leo itakua na kibarua kizito katika dimba la Goodson Park ambapo watashuka dimbani kumenyana na klabu ya soka ya Everton katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.

Manchester United leo itamenyana na Everton ambayo inashika mkia baada ya kupokonywa alama 10 kutokana mashtaka ya matumizi mabaya ya fedha yaliyokua yanawakabili.manchester UnitedMan United wana nafasi ya kuendeleza walichokifanya katika michezo mitano iliyopita katika ligi kuu ya Uingereza, Kwani walifanikiwa kushinda michezo minne kati ya mitano waliyocheza.

Klabu ya Everton wenyewe wamekua na fomu nzuri hivi karibuni licha ya kupokonywa alama 10, Kwani wamefanikiwa kushinda yao miwili kati mitatu ya mwisho waliyocheza na kusuluhu mchezo mmoja.manchester UnitedManchester United leo itakua inanufaika na urejeo wa beki wake wa kushoto raia wa kimataifa wa Uingereza Luke Shaw ambaye alikua anasumbuliwa na majeraha kwa miezi miwili iliyopita, Hivo ni wazi ataongeza nguvu kwenye kikosi cha Man United.

Acha ujumbe