Manchester United Kikaoni Kujadili Hatma ya Ten Hag

Mabosi wa klabu ya Manchester United wameendelea na vikao kwa siku ya pili mfululizo wakijadili hatma ya kocha wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Uholanzi Erik Ten Hag ambaye amekua hana muuendelezo mzuri.

Mabosi wa Manchester United wakiongozwa na Sir Jim Ratcliffe, Dave Braislford, Joel Glazer, Dan Ashworth pamoja na waandamimizi wengine kama kocha wa zamani wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson wameonekana nje ya uwanja wa Old Trafford wakielekea kwenye kikao ambacho kinaelezwa mada kuu ni kujadili hatma ya kocha Ten Hag.manchester unitedMpango unaelezwa ni kuachana na kocha huyo ambaye aliongezewa mkataba mpya dirisha kubwa lililopita ambapo mkataba ungemuweka mpaka mwaka 2026 mwezi Juni, Lakini kutokana na mwanzo mbovu ambao klabu hiyo imeanza nao msimu huu kwenye michuano ya ligi kuu ya Uingereza pamoja na michuano ya Europa.

Kocha huyo ameshindwa kuonesha makali yake ndani ya viunga vya Old Trafford mpaka sasa ndani ya mwaka wake wa tatu wakati ikielezwa amefeli hata kuonesha utambulisho wake wa namna timu inapaswa kucheza kwa maana ya filosofia yake, Hivo wahafadhina wanaona ni kama kocha huyo raia wa kimataifa wa Uholanzi timu imemshinda.

Mabosi wa Manchester United wanaelezwa wameshaanza mazungumzo na makocha mbalimbali kwajili kuchukua kibarua cha kocha Erik Ten Hag, Thomas Tuchel ni moja ya majina ambayo yanatajwa sana kuchukua mikoba ndani ya klabu hiyo lakini kocha ambaye anaelezwa atakaimu nafasi mpaka mwisho wa msimu ni Ruud Van Nestelrooy ambaye kwasasa ni kocha msaidizi klabuni hapo.

Acha ujumbe