Manchester United Kubeba Wawili Bayern

Klabu ya Manchester United ipo mbioni kuwabeba wachezaji wawili wa klabu ya Bayern Munich ambao ni Mathijjs De Ligt pamoja na beki wa kulia Noussair Mazraoui raia wa kimataifa wa Morocco.

Manchester United imekubaliana maslahi binafsi na wachezaji wote wawili hao huku bado kukiwa na mvutano baina yao na klabu ya Bayern Munich ambao wanaelezwa kuhitaji dau kubwa hawa kwa beki Mathhijs De Ligt, Lakini kuna kila dalili mashetani wekundu kukamilisha saini hizo mbili.manchester unitedMan United kwasasa hawana budi kupambana kukamilisha dili la Mathijjs De Ligt kutokana na majeraha ambayo ameyapata beki mpya waliyemsajili klabuni hapo Leny Yoro, Huku beki Mazrauoi yeye akiwa anategemea zaidi kuondoka kwa beki Wan Bissaka ambaye ane yupo mbioni kuondoka ndani ya timu hiyo.

Klabu ya Manchester United inajiamini kua wana uwezo kuwapata wachezaji wote wawili kwakua wachezaji hao wanataka kucheza klabu hiyo De ligt anaisubiri United tangu mwezi Juni, Mazraoui yeye amekataa dili la kwenda West Ham kwasababu ya Man United lakini pia wachezaji hao wanamilikiwa na wakala mmoja anaeitwa Rafaela Pimenta.

Acha ujumbe