Klabu ya Manchester United inaelezwa ina mpango wa kuachana na wachezaji wasiopungua kumi kuelekea dirisha kubwa la mwezi Juni, Katika kuhakikisha wanajenga timu mpya.
Uongozi mpya wa klabu ya Manchester United chini ya mmiliki Sir Jim Ratcliffe wanaamini kuna wachezaji wengi ambao wanapaswa kuondolewa klabuni hapo, Kwakua wanahitaji timu bora na yenye ushindani tena.Kwasasa kuna wachezaji wengi ndani ya klabu hiyo ambao wanapaswa kuondolewa kwakua hawana hadhi ya kuipambania klabu hiyo, Hivo uongozi wa klabu hiyo unaona ni jambo la busara kuhakikisha wanapata wachezaji wengine bora wenye uwezo wa kurudisha ubora wa klabu hiyo.
Klabu hiyo inafahamika ni miaka kumi sasa tangu imeondoka kwenye ubora ambao ilikua nao kipindi cha mkufunzi Sir Alex Ferguson,Kwa kutambua hilo mmiliki mpya anaamini wanapaswa kufanya marekebisho ya haraka ili kuirudisha timu hiyo sehemu wanayostahili kuwepo.Wachezaji ambao wanaelezwa kuchinjwa katika dirisha kubwa ni pamoja na Harry Maguire, Casemiro, Antony, Victor Lindelof, Scott Mctominay, Facundo Pellistri, pamoja Anthony Martial na wengine ambao Manchester United ambao wataonekana wanafaa kuondolewa kadri siku zinavyoenda.