Manchester United Kufanya Mapinduzi

Klabu ya Manchester United inataka kufanya mapinduzi klabuni hapo na hiyo ni baada ya kung’atuka kwa mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo mapema leo Richard Arnorld.

Manchester United imekua kwenye kipindi kigumu kwa takribani miaka 10 wakishindwa kufanya vizuri kwenye michuano mikubwa ambayo klabu hiyo imekua ikishiriki.manchester unitedBilionea Jim Ratcliffe ambaye anatarajia kukamilisha ununuzi wa hisa zake asilimia 25% na bosi huyo ndio inaelezwa anataka kufanya mabadiliko makubwa katika klabu hiyo yatakayoweza kuirudisha klabu hiyo kwenye ubora ambao ilikua nao.

Bosi Jim Ratcliffe ndio inaelezwa ndio amekua kiini cha mabadiliko ya uongozi klabuni hapo, Kwani hata kuondoka kwa mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Richard Arnold yeye ndio amependekeza jambo hilo.manchester unitedManchester United wamemteua Patrick Stewart kama mkurugenzi mkuu wa muda klabuni hapo, Huku Jean Claude Blanc raia  wa kimataifa wa Ufaransa anatarajiwa kua mkurugenzi mpya klabuni hapo msimu ujao.

Acha ujumbe