Manchester United Kumuongezea Mkataba Mainoo

Klabu ya Manchester United ipo kwenye mazungumzo na kiungo wake kinda mwenye umri wa miaka (19) Kobbie Mainoo raia wa kimataifa wa Uingereza ambaye anafanya vizuri ndani ya klabu hiyo kwasasa.

Manchester United kipaumbele chake kwasasa ni kumuongezea mkataba mpya kiungo Mainoo ambaye tangu amepandishwa timu ya wakubwa amekua na msimu bora sana kumfanya mpaka kuitwa timu ya taifa ya Uingereza kwenye michuano ya Euro 2024  na kufanya vizuri pia kwenye michuano hiyo.manchester unitedMpaka sasa hakuna makubaliano baina ya pande zote mbili kwa upande wa klabu na mchezaji lakini upande wa klabu unapambana kwa kiwango kikubwa kuhakikisha kabla msimu haujamalizika wanampa mkataba mpya ambao utakua na maslahi makubwa zaidi ya mkataba ambao anao kwasasa.

Kiungo huyo ambaye amekua na ubora mkubwa sana kwenye klabu hiyo na kua moja ya mhimili kwenye safu ya kiungo ya klabu hiyo licha ya umri wake kua mdogo, Hii imekua sababu kubwa ya klabu ya Manchester United kutaka kumuongezea mkataba kiungo huyo ambaye anatajwa kua na kipaji kikubwa.

Acha ujumbe