Klabu ya Manchester United imeingia kwenye vita na klabu ya Newcastle United kwa ajiri ya kuwania huduma ya kiungo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye anaichezea klabu ya Juventus Adrien Rabiot.
Kunataarifa kuwa klabu ya Manchester United tayari wameshakubaliana na klabu ya Juventus ada ya uhamisho ambayo inakidiria kufikia kiasi £15million.
Awali ilisemekana kuwa Adrien Rabiot anakwenda ndani ya viunga vya St James Park msimu huu kabla ya dirisha la usajiri kufungwa lakini kuingia kwa Manchester United kunaondoa uwezekano wa mfaransa huyo kutua ndani ya viunga vya St James Park.
Japo mtandao wa The Guardian umetoa taarifa kuwa klabu ya Manchester United tayari imeshalipa ada ya uhamisho wa Adrien Rabiot ambauo inakadiriwa kufikia £15million kwa Juventus, ingawa United bado hawajafakiana makubaliano na mchezaji huyo.