Manchester United Kuwapindua tena Milan kwa Fofana

Klabu ya Manchester United ina mpango wa kuingilia dili la klabu ya Ac Milan na kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Youssouf Fofana ambaye anakaribia kwenda Milan.

Manchester United inaripotiwa kujitoa kwenye mbio za kumuwania kiungo wa kimataifa wa Uruguay anayekipiga klabu ya PSG Manuel Ugarte baada ya klabu ya PSG kuhitaji kiwango kikubwa cha pesa ambacho klabu ya Man United imekataa kukilipa, Huku nguvu zikielezwa kuhamia kwa Youssouf Fofana kwasasa ambaye anakipiga klabu ya Monaco.manchester unitedYoussouf Fofana mpaka sasa inaelezwa amefikia kwenye hatua nzuri ya kujiunga na klabu ya Ac Milan akitokea klabu ya Monaco ya nchini Ufaransa, Lakini Man United wanajiamini na wanaona wanaweza kuwapindua Ac Milan na kuweza kumnasa mchezaji huyo kama walivyofanya kwa Joshua Zirkzee.

Klabu ya Man United iliwafanyia ukatili Ac Milan mwezi mmoja nyuma baada ya kuingilia dili la Joshua Zirkzee ambaye alishakubaliana maslahi binafsi na Ac Milan, Lakini wao waliingilia dili na kuweza kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi ambaye alikua anakipiga klabu ya Bologna.

Baada ya dili la Ugarte kuonekana haliwezekani tena Manchester United wanamuona Fofana kama mtu sahihi ambaye atawafaa kuimarisha eneo lao katikati haswa kwenye kiungo wa uzuiaji, Lakini mchezaji huyo ameshakubaliana maslahi binafsi na klabu ya Ac Milan lakini Man United wao wanaamini wana ushawishi na wanaweza kubadili mawazo ya mchezaji huyo.

Acha ujumbe