Klabu ya Manchester United ipo mbioni kumalizana na mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Newcastle United Dan Ashworth ambaye inasemekana yupo tayari kujiunga na mashetani hao wekundu.
Baada ya bodi ya ligi kuu ya Uingereza kupitisha umiliki wa asilimia 25 kwa kampuni ya INEOS chini ya Sir Jim Ratcliffe ambaye ndio mmiliki wa hisa hizo, Kampuni hiyo imeanza kwa kasi kuanza kufanya mabadiliko ya kimfumo ndani ya klabu hiyo.Uamuzi wa kwanza wa kampuni ya INEOS ndani ya klabu hiyo ilikua ni kuachana na mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Richard Arnold ambaye amedumu klabuni hapo kwa muda mrefu, Huku wakimchukua Omar Berrada kutoka klabu ya Manchester City kama mkurugenzi wao wa klabu.
Mabadiliko ya INEOS ndani ya Manchester United hayakuishia kwa mkurugenzi mkuu wa klabu, Lakini klabu hiyo inataka kubadilisha mfumo mzima wa utendaji na kuhitaji timu hiyo kisasa zaidi na ndio sababu ya kufukuzia saini ya Dan Ashworth ambaye yuko ndani ya klabu ya Newcastle kwasasa kama mkurugenzi wa michezo klabuni hapo.Taarifa zinaeleza kua bwana Dan Ashworth ameonesha nia ya kutaka kujiunga na klabu ya Manchester United, Huku kwasasa ikisubiriwa makubaliano baina ya Man United na Newcastle katika kuvunja mkataba wa mtaalamu huyo wa masuala ya michezo kutoka nchini Uingereza.