Klabu ya Manchester United na klabu ya Crystal Palace wamepigwa faini na shirikisho la mpira nchini Uingereza baada ya kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake wasifanye vurugu katika mchezo uliozikutanisha timu hizo katika dimba la Old Trafford.
Manchester United na Crystal Palace wote wamepigwa faini ya paundi elfu hamsini na tano kila mmoja, Na shirikisho la soka nchini Uingereza FA lilitoa angalizo mwezi uliopita kufuatia kilichotokea katika mchezo huo baina ya timu hizo.Tukio lililosababisha kutokea kwa vurugu hizo zilitokea ni baina ya Jeffrey Schlupp pamoja na Antony ambao wote walipata kadi za njano, Lakini pia ilisababisha tukio lililopelekea kufungiwa kwa kiungo Casemiro baada ya kufanya kitendo kischo cha kiungwana mchezoni dhidi Will Hughes.
Fa imesema vilabu hivo kw apamoja vilikubali kua vilishindwa kuhakikisha kua wachezaji wao wanajiepusha tabia za uchochezi michezoni, Hivo kutokana tukio hilo vilabu hivo vilistahili kupata adhabu vilabu vyote kwa pamoja Manchester United na Crystal Palace wakilipa paundi 55,000.Manchester United mbali na kupigwa faini na shirikisho la soka nchini Uingereza FA lakini klabu ya klabu hiyo leo itashuka dimbani katika mchezo wa kombe la shirikisho hilo FA dhidi ya klabu ya West Ham United ambao utapigwa katika dimba la Old Trafford.