Manchester United na Ugarte ni Suala la Muda

Klabu ya Manchester United na kiungo wa kimataifa wa Uruguay Manuel Ugarte ambaye anakipiga ndani ya klabu ya PSG inaelezwa ni suala la muda kwa kiungo kujiunga na Mashetani wekundu.

Manuel Ugarte inaelezwa ameshakubaliana maslahi binafsi na Manchester United na kilichobaki ni klabu hiyo kutoka nchini Uingereza kutoa ofa ambayo itaridhiwa na mabingwa hao wa Ufaransa ili kuhakikisha dili hilo linakamilika siku mapema.manchester unitedManuel Ugarte ni kiungo ambaye yupo kwenye orodha za juu zaidi ndani ya klabu ya Man United na klabu hiyo inahitaji kukamilisha dili la kiungo huyo wa kimataifa wa Uruguay haraka iwezekanavyo, Kwani wanahitaji kukamilisha sajili za wachezaji wanaowataka mapema ili wawepo kwenye maandalizi ya msimu mpya.

Mazungumzo baina ya klabu ya Manchester United na PSG wapo kwenye mazungumzo kwa siku kadhaa sasa kwajili ya kupata hitimisho la usajili wa Manuel Ugarte, Vilabu hivo viwili vikikubaliana itakua jambo jepesi kwa Man United kumpata kiungo huyo kwani kiungo ameshakubali kujiunga na klabu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.