Manchester United ni Majanga Tu

Majanga yanaendelea ndani ya klabu ya Manchester United ambapo imetaarifiwa kua kiungo wao raia wa kimataifa wa Morocco Sofyan Amrabat amepata majeraha tena wakati akiitumikia timu yake ya taifa.

Kiungo Sofyan Anrabat ameripotiwa kupata majeraha ya mgongo ambapo hakushiriki katika mchezo wa jana wa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika kati ya Morocco na timu ya taifa ya Liberia.Manchester UnitedBaada ya taarifa hiyo imeendelea kua chungu ndani ya klabu hiyo kwani siku kadhaa nyuma taarifa zilieleza kua kiungo Casemiro alipata majeraha akiwa anaitumikia timu yake ya taifa ya Brazil, Wakiwa hawajamalizana na taarifa hiyo taarifa za Amrabat kupata majeraha tena zinaibuka.

Mpaka sasa klabu ya Manchester United inakua moja ya timu ambazo zimeandamwa na majeraha zaidi msimu huu, Ikielezwa ni moja ya sababu zilizopelekea klabu hiyo kuanza vibaya sana msimu huu kwenye michuano mbalimbali.Manchester UnitedKiungo Sofyan Amrabat inaelezwa ameshasafiri kurejea klabuni kwake kwajili ya kuchukuliwa vipimo zaidi, Wakati huohuo kiungo Casemiro nae anafanyiwa uchunguzi kutambua jeraha lake ni kubwa kwa kiwango gani hii ni wazi Manchester United msimu huu ni majanga tu.

Acha ujumbe