Manchester United Wapewa Nafasi Kumsajili Vinicius Junior

Manchester United wametajwa kuwa wamepewa nafasi ya kumsajili Vinicius Junior wa Real Madrid.

Kijana huyo wa miaka 21 alikuwa na msimu wa kawaida na Los Blancos kwenye kampeni ya 2020-21, akicheza mechi 49 kwenye mashindano yote.

Lakini Mbrazil huyo anadaiwa kuwepo sokoni msimu huu wa joto, kwani Real Madrid wanataka kuweka sawa vitabu vyao vya fedha kabla ya uwezekano wa kukamilisha uhamisho wa staa wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe.

Manchester United Wapewa Nafasi Kumsajili Vinicius Junior

Man United na Real Madrid tayari wametajwa kuwepo kwenye mazungumzo juu ya Raphael Varane, lakini kwa mujibu wa The Mirror, mabingwa hao wa mara 20 wa Uingereza pia wamepewa nafasi ya kumsajili Vinicius.

Ripoti hiyo inadai kwamba kikosi cha Carlo Ancelotti kinataka Pauni milioni 68.5, lakini Mashetani Wekundu wanaweza kumsaini kwa mkopo kwa kampeni ya 2021-22 na uwezekano wa makubaliano ya kudumu mwaka ujao.

Timu ya Ole Gunnar Solskjaer inadaiwa imeweka wazi kuwa wanavutiwa na mshambuliaji huyo, ambaye amefunga mara 14 na kusajili asisti 23 kwenye mechi 118 za Real Madrid.


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

Acha ujumbe