Manchester United Vs Liverpool Ni Vitaa

Klabu ya Manchester United leo watakua nyumbani katika dimba lao la Old Trafford wakiikaribisha klabu ya Liverpool katika mchezo wa kukata na shoka wa ligi kuu ya Uingereza.

Mchezo kati ya Manchester United na Liverpool mara zote umekua ni mchezo wenye kuvuta hisia kwani timu hizi ni timu zenye uhasimu mkubwa sana nchini Uingereza, Zikiwa ndio timu zenye mafanikio kuliko timu zote.manchester unitedMchezo wa leo utakua muhimu kwa kila timu ambapo upande wa Man United wao watahitaji kutumia mchezo huu kurudi kwenye njia ya ushindi, Huku Liverpool wao wakizihitaji alama tatu za leo ili kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Unaweza kusema Liverpoool ndio wanauhitaji mchezo huu zaidi kwani wako kwenye mbio za bingwa na mpaka sasa wako kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Lakini wakifanikiwa kushinda mchezo wa leo ni wazi watarejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.manchester unitedPale unapofikiria mchezo huu utakua muhimu zaidi kwa Liverpool utakua unakosea kwani hata Manchester United nao mchezo huu ni wa muhimu zaidi kwao, Kwani bado wana ndoto za kushiriki ligi ya mabingwa ulaya hivo watahitaji kushinda mchezo huu ili kuendelea kujiweka kwenye nafasi ya kuendelea kugombea kuwepo kwenye michuano ya ulaya msimu ujao.

Acha ujumbe