Klabu ya Manchester United ambayo inamfukuzia mshambuliaji wa kimataifa Wout Weghorst anayekipa kwa mkopo klabu ya Besiktas ya nchini Uturuki akitokea klabu ya Burnley kwa mkopo.

Baada ya Man United kuhitaji saini ya mshambuliaji huyo Mkurugenzi wa klabu ya Besiktas anayejulikana kama Kazanci ameitaka klabu hiyo kuonana kwanza na klabu ya Burnley kwani wao ndio wamiliki halali wa mshambuliaji Wout Weghorst.manchester unitedMkurugenzi huyo amesema kama Manchester United watawasiliana na Burnley kwanza wakubaliane halafu wawataarifu wao ambao wanammiliki mchezaji huyo kwa mkopo, Na kama wakikubali wanapaswa kuwalipa Besiktas fidia ya kuvunja mkataba wa mkopo klabuni hapo.

Mkurugenzi huyo ameweka wazi kama Manchester United watashindwa kulipa fidia ya kuvunja mkataba wake kwa mkopo ndani ya klabu ya Besiktas, Bai mchezaji hyo atapaswa kusalia klabuni hapo mpaka mwisho wa msimu kumalizia mkopo wake.manchester unitedKlabu ya Manchester United inahitaji mshambuliaji wa kati zaidi kwenye dirisha dogo la mwezi Januari na ndio kipaumbele chao. Mchezaji Wout Wrghorst ndio anatupiwa jicho zaidi na klabu hiyo ili kwenda kuimarisha safu ya ushambuliaji ya mashetani wekundu.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa