Klabu ya Manchester United wamefanya mazungumzo na klabu ya Leicester City ya kuulizia upatikanaji wa mshambuliaji wao nyota Jamie Vardy kwenye majira haya ya kiangazi kabla ya dirisha la usajiri kufungwa.

Jamie Vardy ni miongoni mwa wachezaji ambao wanaweza kuondoka kwenye klabu ya Leicester kabla ya dirisha la usajiri kufungwa, na Manchester United ndio klabu pekee ndiyo imeonesha nia ya kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 35.

Manchester United, Manchester United Wahamia kwa Jamie Vardy, Meridianbet

Manchester United wameweka wazi kuwa wako tayari kumchumkua Vardy, lakini wako tayari kumpa kandarasi ya mwaka moja na si zaidi ya hapo, ila wanaweza kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja mwingine ikiwa atahitajika lakini hicho kipengere hakipaswi kuwepo kwenye kandarasi yake.

Manchester United hivi karibuni walifanya mazungumzo na mshambuliaji wa klabu ya Bologna ili aweze kujiunga na klabu hiyo, lakini alikata offer ya United.

United mpaka sasa washapewa majina ya washambuliaji ambao wanaweza kuwapata kwwenye dirisha hili la usajiri wakiwepo Mauro Icardi na Raul De Tomas, lakini Vardy anapewa kipaumbele kwa sababu ya uzoefu wake kwenye ligi hiyo.

Pia Mpaka sasa klabu ya Leicester City, haijafanya sajiri yoyote kwenye dirisha hili la usajiri huku wachezaji wake muhimu wakiwa njiani kuondoka kwenye klabu hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa