Manchester United bado wanahaha kuipata saini ya mchezaji nyota wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho. United wametolewa nje kwa mara ya kwanza.

Msimu uliopita, United walidhani BVB watalegeza msimamo wao wa kutaka pauni milioni 120 ili kumuachia Sancho. Hakika United walifeli pakubwa, wazungu wanasema “you failed big time”. Baada ya Agosti 10,2020 kupita bila ofa ya kueleweka kutoka United, BVB walitangaza rasmi kuwa Sancho hauzwi tena, ilikuwa hivyo mpaka usajili ulipofungwa.

Msimu huu mambo yamekuwa tofauti kidogo, BVB wamepunguza dau la kumuuza Sancho. Pauni milioni 77 pamoja na bonasi ya pauni milioni 4 zinatosha kumuachia Jadon Sancho. Manchester United bado wanajitafuta kwenye hili, imeripotiwa United wamepeleka dau la pauni milioni 67 ili kumsajili Sancho.

Manchester United, Manchester United Wakataliwa Na Borussia Dortmund., Meridianbet
Sancho anashika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya wachezaji anaowataka kocha, Ole Gunnar Solskjaer kwa msimu ujao.

Dau la United halijaweza kuwatikisa vigogo wa Dortmund ambao kwa sauti moja wamelikataa dau hilo. Japo kuwa Dortmund hawajaweka wazi utaratibu utakaofanikisha usajili wa Sancho, kinachojulikana ni kuwa kuna makubaliano ya awali kati ya BVB na Sancho kwamba mchezaji huyo ataruhusiwa kuondoka Signal Iduna Park endapo timu inayomtaka itafikia vigezo kadhaa.

Upande wa Sancho na wawakilishi wake, United wameshamalizana nao kwa maana ya makubaliano ya awali kwenye vipengele vya mkataba wa miaka 5 (mpaka 2026) kama atajiunga na United. Je, Manchester United watajifikiria zaidi na kufanya maamuzi ya haraka na yenye tija ili kukamilisha usajili wa Sancho au watamkosa kwa mara nyingine?


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa