Manchester United wana imani kuwa watamnasa nyota wa Ajax Antony ndani ya wiki ijayo. Klabu hiyo inaamini kuwa uhamisho huo ulianza tena wikiendi hii baada ya mchezaji huyo kutoa msimamo dhidi ya klabu yake ili kufanikisha mpango huo.

antony,manchester, Manchester United: Wamwanga Mpunga wa Kutosha kwa Antony Santos., Meridianbet

Mbrazil huyo anaonekana kushindwa kuhudhuria mazoezi siku ya Jumamosi na hakuwa sehemu ya kikosi kwenye mchezo wao dhidi ya Sparta Rotterdam.

Winga huyo anataka uhamisho huo utimizwe huku United ikiwa tayari kuongeza ofa yao ya awali ya paundi milioni 68 hadi kufikia pauni milioni 80.

antony,manchester, Manchester United: Wamwanga Mpunga wa Kutosha kwa Antony Santos., Meridianbet

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 atakuwa usajili wa tano katika dirisha hili la uhamisho wa meneja Erik Ten Hag. Pia amekuwa akiitaka bodi kufanya mipango ya kusajili wachezaji zaidi, baada ya kupoteza michezo yao miwili ya ufunguzi wa msimu huu.

Mshambuliaji wa PSV Eindhoven Cody Gakpo anahusishwa na ripoti zinazodai kuwa United walikuwa wamepanga kuweka mkataba wa pauni milioni 34.

antony,manchester, Manchester United: Wamwanga Mpunga wa Kutosha kwa Antony Santos., Meridianbet

Ten Hag pia anatakiwa kukabiliana na hali ya Cristiano Ronaldo, huku mshambuliaji huyo mkubwa akitaka kuondoka katika klabu hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa