Manchester United Yamuongeza Mkataba Tom Heaton

Klabu ya Manchester United imemuongezea kandarasi golikipa wake chaguo la pili ndani ya klabu hiyo Tom Heaton ambapo atasalia klabuni hapo mpaka mwaka 2025.

Tom Heaton ambaye ni zao la akademi ya Manchester United ataendelea kuitumikia klabu hiyo kwa msimu mmoja mwingine mbele, Hivo golikipa huyo ataendelea kua sehemu ya magolikipa wa klabu hiyo akiwa chaguo la pili baada ya Andre Onana na mturuki Altay Bayandir.Manchester UnitedMashetani wekundu wako kwenye mchakato wa kuendelea kukiboresha kikosi chake na moja ni kuhakikisha wanaendelea kuwabakiza wachezaji wake muhimu ndani ya timu, Halafu ndio watafanya usajili wa nje kwa maana ya kusajili wachezaji kutoka vilabu vingine.

Tom Heaton amekua mchezaji wa kwanza wa ndani kuongezewa kandarasi msimu huu wakati ambao klabu hiyo inafanya mazungumzo na wachezaji wengine kuongeza mkataba ndani ya timu hiyo, Lakini pia Manchester United imekua ikihaha kukamilisha sajili mbalimbali kuelekea msimu ujao.

Acha ujumbe