Manchester United ya Asali na Maziwa imerejea

Manchester United ya asali na maziwa imerejea ndio kauli pekee unaweza kuitumia kwasasa ambapo klabu hiyo leo imetimiza mchezo wake saba bila kupoteza kwenye michuano yote baada ya kuibamiza Everton katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.

Klabu ya Manchester United leo imefanikiwa kupata ushindi mnono kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya klabu ya Everton baada ya kuikung’uta klabu hiyo kwa jumla ya mabao manne kwa bila, Ikiwa ni ushindi mnono zaidi walioupata klabu hiyo baada ya kupita muda mrefu kwenye ligi kuu ya Uingereza.manchester unitedMan United waliuanza mchezo kwa kasi na kuonesha wana nia ya kupata mabao mapema na walionekana kufanikiwa kwani walipata mabao mawili kipindi cha kwanza kupitia kwa Marcus Rashford na Joshua Zirkzee usajili mpya klabuni hapo na kipindi cha kwanza kikimalizika wakiwa mbele kwa mabao mawili.

Mashetani wekundu waliingia kipindi cha pili wakiendelea walipoishia kipindi cha kwanza ambapo mapema tu dakika ya 46 Marcus Rashford aliipatia United bao la tatu akipokea pasi safi ya Amad Diallo, Vijana wa Ruben Amorim waliendeleza msako ambapo mnamo dakika ya 64 Zirkzee alifunga bao la nne na kukamilisha karamu ya magoli kwa klabu hiyo.manchester unitedManchester United baada ya ushindi wa leo wamefanikiwa kupanda mpaka nafasi ya 9 kutoka nafasi ya 12 ambapo wamefikisha jumla ya alama 19 huku magoli ya kufunga na kufungwa pia yakipanda mpaka manne, Kwani walikua 0 kwa muda mrefu kibarua kinachofuata kwa United ni Emirates dhidi ya Arsenal.

Acha ujumbe