Manchester United Yahusishwa na Onana wa Everton

Klabu ya Manchester United imeanza kuhusishwa na kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji Amadou Onana ambaye anakipiga katika klabu ya Everton inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.

Amadou Onana amekua kwenye kiwango kizuri ndani ya klabu ya Everton tangu ajiunge na klabu hiyo jambo ambalo linaelezwa kuwavutia maskauti wa Manchester United na kumuweka mchezaji huyo kwenye orodha ya wachezaji wanaowataka katika dirisha kubwa.manchester UnitedMan United hawatakua wenyewe katika mbio za kumuwania kiungo huyo mwenye kimo kizuri anayesifika kwa uwezo wake wa kukaba, kuzunguka eneo kubwa la uwanja, lakini pia kushinda mpambano wa juu na chini, Kwani vinara wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Arsenal nao wanatajwa kuvizia saini yake.

Arsenal wanamuona kama mchezaji ambaye anaweza kushirikiana vizuri na kiungo wao Declan Rice klabuni hapo na kutengeneza moja ya viungo vigumu zaidi, Lakini Man United wao wanaona ni mshirika mzuri wa kijana wao Kobbie Mainoo anayefanya vizuri kwenye eneo la katikati.manchester UnitedKiungo Amadou Onana ndio kwanza ana miaka (21)jambo ambalo linafanya timu nyingi kuona ni wakati sahihi wa kumchukua mchezaji huyo kutokana umri wake kushawishi, Manchester United wao wanaona watatengeneza kiungo ambacho kitadumu kwa muda mrefu klabuni hapo kwani Mainoon ana miaka (18)huku Onana akiwa na miaka (21).

Acha ujumbe