Manchester United Yakamilisha Uchunguzi Salata la Greenwood

Klabu ya Manchester United imeto taarifa kwa umma kua imefanikiwa kukamilisha uchunguzi juu ya sakati lililokua linamkabili mshambuliaji wa klabu hiyo Mason Greenwood.

Manchester United imeweka wazi kua imeshakamilisha uchunguzi wao juu ya sakata la unyanyasaji wa kijinsia ambao alikua anashutumiwa nao Mason Greenwood, Huku wakiweka wazi wako kwenye hatua za mwisho katika kufanya maamuzi.Manchester UnitedKlabu hiyo iliahidi kufanya uchunguzi binafsi baada ya mahakama kupiga chini mashtaka yaliyokua yanamkabili Greenwood baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha, Hivo klabu hiyo leo jioni imesema kwasasa ipo kwenye hatua za mwisho kuhakikisha wanatoa maamuzi juu ya mustakabali wa mchezaji huyo klabuni hapo.

Klabu ya Man United imeweka bayana kua taarifa zinazosambaa mitandaoni kua maamuzi tayari yameshafanywa na klabu hiyo ni za uongo, Kwani kwasasa ndio wamekamilisha uchunguzi wao na wako kwenye hatua za mwisho kwenye kufanya maamuzi ambayo yatafanyiwa kazi na mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo.Manchester UnitedKlabu ya Manchester United wamekiri kua suala la kufanya maamuzi juu ya mchezaji Mason Greenwood ni jambo ambalo limekua gumu zaidi kwa yeyote ambaye anahusishwa na klabu hiyo, Lakini watatoa maamuzi hivi karibuni na kuwahamisha watu wote.

Acha ujumbe