Klabu ya Manchester United imekanusha kuwepo kwa mpasuko katika vyumba kubadilishia nguo vya klabu hiyo baada ya kupokea kichapo katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Brighton.
Wachezaji wanne wa klabu ya Manchester United waliripotiwa kuingia kwenye mazozano baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Brighton siku ya Jumamosi na wachezaji hao ni Bruno Fernandes, Scott Mctominay, Victor Lindelof na Lisandro Martinez.Klabu hiyo inaelezwa kukanusha taarifa hizo zilitoka za kutokuelewana kwa wachezaji kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kuweka wazi hali ni shwari na wamejiandaa kikamilifu kuelekea mchezo wao kesho dhidi ya Bayern Munich.
Man United ni wazi hawajaanza vizuri katika ligi kuu ya Uingereza ambapo mpaka sasa wameshapoteza michezo mitatu kati ya mitano ambayo wamecheza, Huku kesho wakitarajia kukipiga dhidi ya Bayern Munich katika mchezo wao wa kwanza wa ligi ya mabingwa msimu huu.Taarifa za ndani kutoka ndani ya Manchester United zinaeleza kua sio kweli juu ya taarifa zinazosambaa kua klabu hiyo imekua kwenye malumbano, Zaidi timu hiyo inatazamia namna ya kuikabili michezo iliyopo mbele yao zaidi.