Manchester United Yamuwinda Kiungo Spurs

Klabu ya Manchester United imeingia kwenye mawindo ya kumuwinda kiungo wa klabu ya Tottenham Hotspurs raia wa kimataifa wa Denmark Pierre Emile Holjberg.

Manchester United wana orodha ya wachezaji kadhaa katika nafasi ya kiungo kama Sofyan Amrabat na kiungo Pierre Emile Holjberg ameingia kwenye orodha hiyo anaonekana kama moja ya machaguo ambayo yanapewa nafasi kubwa.Manchester UnitedMan United wameulizia huduma kiungo huyo wa kimataifa wa Denmark ambaye amecheza katika ligi kuu ya Uingereza kwa misimu kadhaa katika vilabu viwili na kuwafanya United kuamini ni moja ya machaguo mazuri kutokana na uzoefu aliokua nao.

Faida inaweza kuwakuta pia mashetani wekundu kwaku Holjberg haonekani kama chaguo la kwanza la mwalimu ndani ya klabu hiyo, Hivo kitendo hichi kinaweza kurahisisha Man United kumshawishi kiungo huyo aweze kuungana nao.Manchester UnitedDirisha kubwa la majira ya kiangazi limebakiza siku tatu kuweza kumalizika Manchester United wanapaswa kufanyia kazi orodha yao katika siku hizi tatu kwajili ya kuhakikisha wanakamilisha usajili wa kiungo Pierre Emile Holjberg.

Acha ujumbe