Manchester United Yarejea kwa Yoro

Klabu ya Manchester United imerejea kwenye mbio za kumuwania beki Leny Yoro raia wa kimataifa wa Ufaransa ambaye anakipiga kwenye klabu ya Lille ya nchini humo.

Manchester United leo wamepeleka ofa rasmi kwa klabu ya Lille ya kiasi cha €50 milioni na klabu hiyo imekubali dau hilo, Lakini beki  huyo ndio anasubiriwa kukubali ili klabu hiyo iweze kumpiga bei kuelekea kwa miamba hiyo ya soka nchini Uingereza klabu ya Man United.manchester UnitedChangamoto inaelezwa mpaka sasa ni upande wa mchezaji ambaye inaelezwa chaguo lake la kwanza limekua klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania jambo ambalo limekua likifanya dili hilo kuchelewa, Kwani mpaka sasa klabu ya Lille imekubali ofa ya Mashetani wekundu.

Klabu ya Real Madrid ndio imekua changamoto kwenye dili kwa upande wa Manchester United kwakua mchezaji huyo kipaumbele chake cha kwanza ni mabingwa hao wa soka nchini Hispania, Lakini klabu ya Lille wanamsisitiza beki huyo akubali ofa ya United kwakua ndio ofa nzuri iliyo mezani kwao.

Acha ujumbe