Manchester United Yashinda Kibabe

Klabu ya Manchester United imefanikiwa kupata matokeo ya ushindi kibabe wakiwa ugenini katika dimba la Goodson Park baada ya kuitandika Everton kwa mabao matatu kwa bila.

Manchester United kwenye ubora mkubwa wanafanikiwa kushinda mchezo wa pili kwa mabao mengi, Hii ikiwa ni baada ya mchezo dhidi ya Nottingham Forest ambapo walishinda kwa mabao matatu kwa moja.manchester UnitedMchezo huo ambao uliishuhudia Man United wakipata goli mapema kabisa dakika ya tatu ya mchezo ambalo lilifungwa na Alejandro Garnacho kwa staili ya aina yake akifunga goli la tiktaka ambalo liliwapa klabu hiyo mpaka kufikia mapumziko.

Klabu hiyo iilrejea kipindi cha pili ikionekana kuhitaji kuongeza bao la pili lakini wenyeji klabu ya Everton nao wakionekana kutafuta bao la kusawazisha mpaka pale Ashley alipofanya makosa na kusababisha penati iliyofungwa na Marcus Rashford na kuwapa United bao la pili.manchester UnitedManchester United baada ya ushindi wa leo sasa wanakua wameshinda michezo mitano mfululizo ya ligi kuu ya Uingereza mpaka, Huku wakikusanya alama 15 wakati huo klabu hiyo imefikisha alama 24 wakiwa nyuma kwa alama sita dhidi ya vinara klabu ya Arsenal wenye alama 30.

Acha ujumbe