Klabu ya Manchester United imefanikiwa kupata ushindi katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Leicester City mchezo uliopigwa katika dimba la Old Trafford mapema leo.

Manchester United wameibamiza klabu ya Leicester kwa jumla ya mabao matatu kwa bila huku mshambuliaji hatari klabuni hapo kwasasa Marcus Rashford akiendelea kuwasha moto, Rashford amefanikiwa kufunga mabao mawili katika uhindi huo huku Sancho akifunga bao moja.manchester UnitedMashetani wekundu wamefanikiwa kufikisha alama 49 baada ya kushinda mchezo wa leo dhidi Leicester na kupunguza pengo la alama baina yao na kinara Arsenal kufikia tano huku wakibakiza alama tatu kwa wanakamata nafasi ya pili klabu ya Manchester City.

Marcus Rashford yeye anaendelea kutakata tu ndani ya Manchester United kwani mpaka sasa amefanikiwa kukwamisha mpira wavuni mara 24 kwenye michuano yote na jumla ya pasi 8 za mabao, Mchezaji huyo amekua na kiwango bora sana msimu huu huku akivunja rekodi yake mwenyewe baada kufikisha magoli 24 ambayo hajawahi kufika.manchester UnitedKlabu ya Manchester United wao wanaendelea na rekodi yao ya kutopoteza nyumbani katika michezo yao, Mpaka sasa wakiwa wameshacheza michezo 18 katika dimba la Old Trafford huku wakishinda michezo 17 na kusuluhu mchezo mmoja ikiwa ni rekodi bora zaidi tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa