Klabu ya Manchester United imefanikiwa kushinda mchezo wake wa pili mfululizo kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kuifunga klabu ya Luton Town bao moja kwa bila.

Manchester United wakiwa katika dimba lao la nyumbani la Old Trafford wamefanikiwa kupata alama tatu muhimu baada ya kuifunga klabu ya Luton Town ambao wametoka kusuluhu na Liverpool wikiendi iliyopita.manchester unitedMashetani wekundu waliutawala mchezo huo kwa kiwango licha ya kua wamepata ushindi mwembamba wa bao moja kwa bila mbele ya Luton Town katika mchezo huo wa ligi kuu ya Uingereza.

Victor Lindelof ndio alihakikisha Man United wanapata alama tatu kwani ndie aliyefunga bao pekee lililoipa ushindi klabu hiyo, Licha ya ushindi lakini Man United wanaonekana bado kuchechemea na hawajarudi kwenye ubora wao.manchester unitedBaada ya mchezo wa leo ligi itasimama kwa muda kupisha michezo ya kimataifa, Hivoo hii inaweza kua nafasi nzuri kwa Manchester United kujitafakari na kurudi na kasi baada ya mapumziko ya michezo ya kimataifa.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa