Manchester United Yatangaza Kikosi Cha Pre-Season

Klabu ya Manchester United imetangaza kikosi chake cha wachezaji 26 ambao watakwenda nao kwenye pre-season ambayo wataanzia nchini Norway.

Manchester United kesho itakua imefika katika jiji la Oslo nchini Norway ambapo watapiga mchezo wa kirafiki wa kwanza ambapo watamenyana na klabu ya Leeds United ambayo imeshuka daraja na ipo kwenye Championship kuelekea msimu ujao.Manchester UnitedKikosi cha wachezaji 26 ambacho kimetangazwa na klabu hiyo kuelekea kuanza maandalizi ya msimu kimekua na vijana wengi kuliko wachezaji wa kikosi cha kwanza ambapo wachezaji nguli wengi wakiwa hawajajiunga na timu hiyo.

Wachezaji kadhaa wa timu ya kwanza ambao hawajajumuishwa kwenye kikosi kama Rashford, Bruno Fernandes, Diogo Dalot, Tyrell Malacia na Victor Lindelof wataungana na timu siku za mbeleni ambapo tayari timu itakua imeshaanza maandalizi.Manchester UnitedManchester United ambayo imetangaza kikosi chake ambacho kitaelekea kwenye maandalizi ya msimu ujao, Wachezaji wawili Donny Van de Beek na kipa Deah Henderson hawajajumuishwa kwenye kikosi hicho jambo ambalo linatoa ishara kua wachezaji hao wanmaweza wasibaki ndani ya timu hiyo.

 

Acha ujumbe