Roberto Mancini amesifia kizazi kipya cha Italia kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya England katika Ligi ya Mataifa. Goli la Giacomo Raspadori liliifanya England kushuka daraja, huku Italia itamenyana na Hungary Jumatatu kuamua nani atafuzu fainali za ligi ya Mataifa.

 

Mancini Aisifia Italia

Baada kushindwa kufuzu kwa kombe la Dunia nchini Qatar, Mancini ameangalia wachezaji wachanga kwa siku za usoni huku Raspadori mwenye umri wa miaka 22 akionekana kuwavutia mabingwa hao wa Ulaya.

“Tulianzisha mwezi Juni na mara zote tulikuwa kwenye mbio za kundi hili la ligi ya Mataifa. Ni wazi, tunahitaji michezo hii, ushindi huu, ili tuweze kukua, alisema;

“Nilitarajia utendaji mzuri na nilijua itakuwa ngumu, kwasababu vijana wengi , usliku wa leo hawakuwa na uzoefu katika kiwango hiki, na hakuna hata asilimia 30 ya mechi za England, Lakini nadhani tulishinda kwa kustahili.

Mancini Aisifia Italia

Mancini aliulizwa; ni kwanini Italia wanaonekana kuwa wafanisi zaidi wanapokuwa chini ya shinikizo kuliko katika michezo ambayo wanapenda sana lakini hakukubali kuwa ndivyo ilivyokuwa.

“Sidhani kama hatujatupa chochote”  soka lina kila kitu cha bahati, tulishinda Euro kwa mikwaju ya penati, tulistahili kushinda, kisha tukashindwa kufuzu kombe la Dunia baada ya michezo miwili tuliyoitawala na hatukushinda dhidi ya Uswiz,” alieleza.

Kuhusu England, Mancini anasalia na imani kwamba kikosi cha Gareth Southgate kinaweza kuwa washindani kwenye kombe la Dunia nchini Qatar.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa