Taarifa mbalimbali zinadai kuwa Mchezaji wa Liverpool, Sadio Mane yupo tayari kuondoka katika klabu ya Liverpool kwenye Dirisha hili la usajili baada ya kukaa klabuni hapo kwa miaka sita.
Tetesi ziliaanza kusambaa kabla ya Liverpool kucheza fainali ya llabu bingwa ulaya dhidi ya Madrid, lakini Mane alisema ataweka wazi kama ataondoka au la baada ya mchezo huo.
Sadio alijiunga na Liverpool June, 2016 akitokea Southampton kwa dau la £34 million na kusaini mkataba wa miaka 5.
Bayern Munich ndio klabu inayoongoza mbio za kumuwania Mane japo inaelezwa kuwa bado timu nyingine zinaweza kuweka dau la kutaka kumsajili mchezaji huyo wa Kimataifa wa Senegal.
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!