Mchezo wa masumbwi umekuwepo kwa mda mrefu sana hadi sasa. Boxing inatajwa kuwa ilianzishwa kitambo na vizazi vya kale vya Ugiriki, jamaa waliamua kutupiana migumi ya uso ili kufurahisha umati wa watazamaji na kujipatia kipato.
Mchezo huu ulipitia panda shuka kadhaa na maboresho kutoka kizazi kimoja hadi kingine mpaka leo hii tunazungumza Boxing inayofuatiliwa na mamilioni ya watazamaji ulimwenguni.
Mchezo huu umekuwa ni moja ya michezo maarufu zaidi ya wakati wote katika historia ya binadamu. Wataalamu wa mambo wanasema kuwa mchezo huu ni jaribio kubwa kwa binadamu, pale unapowekwa ulingoni pamoja na mwenzako na kuambiwa uchague kufurahia raha na utamu wa kushinda au uchungu na maumivu ya kushindwa.
Kwa mda mrefu, Boxing imehusisha mechi nyingi sana kubwa katika ulimwengu huu. Lakini katika kila zuri na bora, kuna bora zaidi. Watu tofauti wamezitaja mechi zao wanazoona ziliwahi kutisha zaidi, mechi kubwa zaidi katika historia. Lakini hapa tunakusogezea mechi zako 3 maarufu na kubwa zaidi kwenye rekodi ya Masumbwi
Floyd Mayweather vs Manny Pacquiao:
Ilikuwa maeneo ya MGM Grand Garden Arena, Las Vegas, Nevada mwaka 2015. Hili watu huliita pambano la karne. Wakati Floyd Mayweather kutoka Ardhi ya Marekani akitupiana migumi na Manny Pacquiao kutoka Ufilipino. Linasimama kama Pambano kubwa lililokusanya pesa nyingi sana katika historia ya boxing likikusanya Dola Milioni 410.
Muhammad Ali vs Joe Frazier
Hii ilikuwa Araneta Coliseum, Manila, Ufilipino Oktoba 1975. mika hii kisingeli hakikuwepo hata kwenye ndoto za waswahili hapa bongo, au siyo! Hili lilikuwa ni pambano la mwisho katika mapambano 3 ambayo Muhammad Ali na Joe Frazier walikutana ulingoni. Ni pambano maarufu kwa jina la “Thrilla in Manilla”. Katika pambano hili Ali alishinda kwa TKO, Frazier aligalagazwa chini na kushindwa kuitikia kengele 15 za uamuzi.
Sugar Ray Leonard vs Tommy Hearns
Hili lilikuwa pale Caesar Palace, Las Vegas, Nevada ni mwaka1981. Wakati huo Leonard akiwa na miaka 25 alipanda ulingoni na mtaalamu wa KO Hearns aliyekuwa na miaka 22 tu wakati huo. Hapa mshindi alikuwa anapewa taji la WBA na Ubingwa wa dunia wa WBC -Welterweight. Leonard alimshinda Hearns katika raundi ya 14, na pambano lilikonga nyoyo za wapenda masumbwi na kubaki kuwa moja ya mapambano yanayokumbukwa katika historia ya masumbwi.
Hope mwaikuka
Nomaa sana
Emmy cleopa
Habar njema
Adelta
Hatari sana
David pere
Duuh nilikuwa sijui kabisa asanteni sana
Povel
Duh nilikuwah cjui thnks meridian bet kwa kutupa update za masubwi(ndonga) za nyuma
Theckla
Huu mchezo umekuwa maarufu Sana duniani
aisha
Duuh ilikuwa balaa zito
Ernest
Asante Meridianbet kwa kutujuza sisi watoto wa 2000 hapa
Antony Luseno
Duh katika aya matatu hamna la `iron mike`
Dickson.K
Mike ni bondia maarufu, wajuaji wa ndondi wanasema alikuwa maarufu kuliko ubora wake. Hajaingia hata kwenye 10 bora za wanandondi bora wa wakati wote.
Khadija
Duuh ilikuwa noma sana#meridianbettz
Neema hassan
Asante kwa makala#meridianbet
Tahiya
Duuh atarii sana
Theonestina
Asante meridianbet kwa taarifa
Mwanaidi
Mapambano ya kibabe
Salma
Ilikuwa hatari
Samiah
Nihatari sana
Rehema Dickson
Balaa zito
Lydia Emmanuel Magoti
Noma sana
Furahav
Ilikuwa noma sana.
Mariam mtandama
Duuuh
frank patrick
Kumbe Tyson vs Evanda na yale Tyson vs Lenox Lewis yalikuwa chamtoto tu eenh
Warda
Noma sana hii#Meridianbettz
Ester mmakasa
Ni kweli ilikuwa balaa hatari.
Mwajuma
Du ilikuwa balaa
Gabriel
Hatar sana
dorophina
Mapambano ulikuwa wa kibabe sana
Hamidu
Meridianbet mpo vizuri kwa habari za michezo.
Lombo
mambo ya masumbwi
Rehema
Hii ni gemu hatari
felister
nilikua silifahamu ilo ahsent meridianbet kwa kutujuza
Carolyne
Atari atari hii
SADICK
Ebwanaee hapana jua hii kitu. Ni mchezo wa kusisimua sana. Asante kwa makala ya uhondo wa masumbwi #Meridianbettz
Evaluziga
Duh ni hatari sana
Ester
Aaah sikulijua hili asante sana meridian
Tatu
Habari nzuri
Kenani
Good news
Amani
Asante kwa makala#meridianbet
Neema juma
Balaa tupuu
Mwanahamisi
Hatari sana
winfrida
pambano lilikuwa nomaa
Genia skaluzwe
Hii mechi ngum sana
Genia skaluzwe
Hii mechi ilikuwa gumu sana
Agness
Duuh hatari sana
mwakalosi
hii article safi sana
Elika
Hilo pambano lilikuwa sio la kitoto