Kwa miaka ya hivi karibuni, Manchester United imekuwa na misukosuko ya kila namna, ndani na nje ya uwanja. 2021/22 mapinduzi yameanza.

Toka Sir Alex Ferguson amestaafu kuiongoza klabu hiyo, Man United imeshabadilisha jumla ya makocha 4 na sasa wanamkabidhi timu kocha wa 5 ndani ya miaka 10. Pamoja na kubadilisha makocha, United hawajatwaa taji la EPL wala kuwa na uhakika wa kupambania taji hili na mengine mengi. Hii sio kawaida ya The Red Devils, imekua ni timu dhaifu ndani ya miaka 10.

Mabadiliko yalikua yakifanyika kwenye benchi la ufundi na wachezaji tu, mfumo huu haujazaa matunda muda wote huo, hali imezidi kuwa mbaya. Safari hii, mabadiliko ya benchi la ufundi yanaendana na mapinduzi ya uongozi wa klabu hiyo.

mapinduzi, Mapinduzi Makubwa Man United., Meridianbet
Ed Woodward.

Alianza Mtendaji Mkuu – Ed Woodward, wakafata waandamizi wa idara ya usajili na ufatiliaji na sasa, kiongozi wa idara ya majadiliano na ufatiliaji ameachia ngazi. Hizi ni nafasi 3 ambazo zimekua zikifanya kazi kwa karibu zaidi ndani ya miaka 10.

Pamoja na kuondolewa/kuondoka kwa watu hawa, United imeweka mifumo mipya ya kiutendaji ikiwa ni pamoja na kuwekwa kwa nafasi maalumu za soka kwenye mfumo wa uongozi – Mkurugenzi wa Soka na Msimamizi wa Ufundi ni miongoni mwa nafasi hizi ambazo hazikuwepo klabuni hapo.

mapinduzi, Mapinduzi Makubwa Man United., Meridianbet

Mapinduzi yameenda mbali zaidi, kocha mpya anayetarajiwa kuanza kazi mwishoni mwa msimu huu – Erik Ten Hag, kwa mara ya kwanza, anapatiwa nafasi ya kuwa na kura ya maamuzi kwenye dirisha la usajili. Atakua akifanya kazi kwa ushirikiano wa karibu zaidi na bodi ya wakurugenzi pamoja na watu wenye weledi wa soka kwenye klabu hiyo. Hii haikuwahi kutokea toka enzi za Fergie.

mapinduzi, Mapinduzi Makubwa Man United., Meridianbet
Glazers.

Japokuwa michakato hii inaendelea kuonesha mwangaza kwa mashabiki wa United, bado kunavuguvugu kali la kutaka mapinduzi zaidi katika ngazi ya umiliki wa klabu. Mashabiki wanaendelea kuandamana wakishinikiza familia ya Glazers kuachia ngazi kwenye klabu hii ambayo wamekua wakiimiliki toka 2005. Kwa lugha nyepesi, mashabiki wa United hawana imani na wamiliki wa klabu yao ambayo inapotea kwenye dira ya soka duniani.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa