Beki mkongwe wa Brazil, Marcelo amethibitisha kuwa anaondoka Real Madrid baada ya ushindi katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Marcelo, 34 amekuwa na Los Blancos tangu 2007, akicheza mechi 550 akiwa na klabu hiyo akifanikiwa kushinda mataji 25 akiwa ni mchezaji aliyetwaa mataji mengi ndani ya klabu hiyo.

 

marcelo, Marcelo Athibitisha Kuondoka Madrid Baada ya Miaka 15., Meridianbet

Baada ya ushindi wa jana dhidi ya Liverpool beki huyo alithibitisha kwamba ataondoka ndani ya klabu hiyo msimu huu baada ya miaka 15 mkataba wake unamalizika mwezi Juni.

“Ilikuwa mechi yangu ya mwisho na Real Madrid,” Marcelo alisema.

Miongoni mwa mafanikio yake ni pamoja na mataji matano ya Ligi ya Mabingwa, Vikombe vinne vya Kombe la Dunia la Vilabu, Makombe matatu ya Super Cup ya Ulaya, sita ya La Liga, mataji mawili ya Copa del Rey na matano ya Super Cups ya Uhispania.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa