Maresca: Tunaweza Kusajili Mshambuliaji

Kocha wa klabu ya Chelsea Enzo Maresca anasema milango ipo wazi bado kwa klabu hiyo kuweza kusajili mshambuliaji mpya ambaye anaweza kuwasaidia katika eneo hilo.

Kocha Maresca wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari leo aliulizwa juu ya kuongeza mshambuliaji kwenye klabu yake na majibu yalikua hivi “Iwapo tutapata nafasi ya kumsajili mchezaji wa namba tisa ambaye anaweza kutusaidia na kufanya mabadiliko… basi, tutajaribu.”marescaLicha ya klabu ya Chelsea kufanya usajili wa wachezaji wengi lakini bado safu yao ya ushambuliaji inaonekana kua na mapungufu jambo ambalo linafanya klabu hiyo kufikiria kutafuta mshambuliaji mwingine sokoni ambaye atakua na ubora mkubwa na kuleta utofauti ndani ya timu hiyo mpaka sasa.

Kutokana na kauli ya kocha Enzo Maresca inaonesha wazi bado hafurahishwi na mwenendo wa washambuliaji wake wawili klabuni hapo Nicklas Jackoson, na Christopher Nkunku hivo kama itatokea fursa ya kuingia sokoni na kusajili mshambuliaji bila shaka kocha huyo atafanya hivo.

Acha ujumbe